Viongozi, mastaa watoa maoni yao kufuatia Nape kupokonywa uwaziri, wengi wamuita ‘shujaa’
Alhamis hii jua limechomoza likiambatana na mshtuko mkubwa kwa wananchi wengi wa Tanzania. Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito. Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo. Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa. Haya ni baadhi yao: Zitto Kabwe Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shuja...

Comments
Post a Comment